Makaburi ya pamoja ya mamia ya raia waliouwa katika machafuko nchini Burundi yamegundulika hivi karibuni kupitia picha za ‘Satelaiti’.

Shirika la Kimataifa la Amnesty International limeeleza kuwa limepata picha za ‘satelaiti’ zinazoonesha mamia ya raia wakiuawa na baadae kuzikwa katika makaburi ya pamoja katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura.

Amnesty International wameeleza kuwa uchunguzi wao umeoana na maelezo ya mashahidi waliodai kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouawa tarehe 11, Desemba mwaka jana baada ya kuzuka machafuko kati ya watu wanaopinga utawala wa Rais Pierre Nkurunzinza na vyombo vya dola.

Umoja wa Afrika unakutana nchini Ethiopia kujadili mgogoro huo wa Burundi pamoja na kutoa msimamo wake kuhusu katazo la rais Nkurunzinza kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa kuingia nchini humo kulinda amani.

Justin Bieber ageuka shujaa, amuokoa mwanamke barabarani
Muigizaji wa ‘Titanic’ akutana na Papa Francis kwa sababu hii

Comments

comments