Ukitazama kiwanda cha kuzalisha vijana cha @azamfcofficial unaweza ukajiuliza kuna sababu yangu ya kuwavumilia Ma pro wasio na matokeo ndani ya kikosi chao.

Miaka ya hapa karibuni @mtibwaofficial Imejibebea sifa kubwa kwa kuzalisha vijana wengi walio bora na wenye kiwango bora ambao 80% mpaka 90% leo hii wanatazamwa kama tegemezi kwa Taifa kama vile Dick Job, Kibwana shomari, Nick Kibabage, Frank Kahole, Abtwalibu Mshery na Joseph Mkele.

Azam FC nao wakaja wakapita njia zile zile za kuwaimarisha kiwanda chao nao wakatoa vijana wengi sana na bora kama Oscar Masai, Tepsi Evance,Paul Peter,Lusajo Mwaikenda,Onditi na hata Pascal Msindo.

Changamoto kwa Azam Fc hapo nyuma walikuwa hawana imani na vijana wao ila wanapo watoa kwa mkopo wanakuta wanaaminiwa sana na wanaleta mafanikio ugenini kwa Mfano Oscar Masai aliondoka kwa mkopo Azam Fc na kujiunga @namungofc akawasaidia kuwapandisha ligi kuu huku Namungu wakiwa wameruhusu goli chache zaidi.

Lusajo Mwaikenda akiwa na @kmcfc_official Msimu uliopita,alifanya makubwa sana akisimama imara kwenye ulimzi na kisha kumrejesha.

Msimu huu wameingiwa na imani ya kuwaamini vijana wao na tayari wameshaanza kuwapa matokeo kwenye michezobali mbali kama vile ya ligi kuu, FA na hata Mapinduzi cup

Maoni yangu: Kama unamvumilia Mchezaji wa kigeni kwanini ushindwe kumvumilia kijana aliyetoka kwenye taasisi yako ? Sidhani kama Azam wanahitaji beki mwingine wa kati kwakuwa ukiwatazama wanakiwanda kikubwa sana cha vijana walio bora.

WALINZI
Oscar masai, Lusajo Mwaikenda na Pascal Msindo

USHAMBULIAJI
Andrew simchba, Paul Peter na Tepsi Evance

Nadhani kama Azam ni muda wakurudisha matumaini yao 100% kwa vijana wao kwakuwa wengine wana vitu kuzidi hata hao ma pro, JIULIZE NAFASI ANAYOPATA MBOMBO VIPI ANGEPEWA PAUL PETER angekuwa na goli ngapi?
SIMAANISHI KUWA MAPRO HATAKIWI, NO! namaanisha kwa mapro waliopo 70% ni kheri mkawarudisha vijana wetu wakaja kuifanya ambayo wanafanya mapro kama zulu,Mbombo na kola pia.
Ameandika @nestory_tweve05

Chama awavuruga Mashabiki
TPLB yafanya mabadiliko Ligi Kuu