Katika pitapita zako lazima utakuwa umewahi kukutana na neno linalosema ”Beuty with Brain” kwa tafsiri ya lugha mama ”Kiswahili” linaweza someka ”Urembo na Utashi” neno hili hutumika zaidi kwa wasichana warembo wenye akili na mafanikio kimaisha.
Kibongo bongo naweza wataja wadada wachache ambao kwa maono yangu ni ”Beauty with Brain”
Jackline Ntuyabaliwe huyu ni mrembo msomi ambaye amewahi kutwaa taji la Umiss Tanzania mwaka 2000 lakini hakuishia hapo ameolewa na moja ya matajiri hapa nchini Reginald Mengi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Media, lakini mbali na hilo huyu dada ni mbunifu, mfanyabiashara na mwanamitindo mashuhuri hapa nchini, sio mtu wa ‘scandal’ kama ilivyo kwa wadada wengine waliojipatia umaarufu hapa nchini.
Flaviana Matata, huyu dada ni miongoni mwa warembo tunaoweza kuwatunuku taji la Ubeuty with Brain kwasababu ni miongoni wa warembo wenye mafanikio makubwa hapa nchini kupitia sanaa yake ya ubunifu na uwanamitindo ambayo imeweza kumtembeza karibu dunia nzima, amewahi kushiriki na kutwaa taji la Umiss Universe, ni moja kati ya watoaji wazuri wa misaada kwa watu mbalimbali hapa nchini hasa watoto.
Wengine ni Vanessa Mdee, Shilole, Jokate Mwagelo, Faraja Nyalandu, Zarinah Hassan na wengine wengi ambao ni wadada wenye urembo, utashi na mafanikio makubwa na ya kuigwa.
Kwa upande mwingine dhima hii hutumika vibaya na wadada wanaojitambua ni wenye mvuto kimaumbo, kisura na hata kiakili hutumia vibaya uzuri wao kwa kufanya mambo ambayo hayakubaliki katika jamii.
Wengi wao wamekuwa wavivu kujishughulisha katika mambo mbalimbali ya kuwatengenezea kipato na kugeuza miili yao kama mtaji wa kupatia pesa.
Hivyo ni chukue fursa hii kutoa ushauri kwa wadada ambao wanatumia uzuri wao kama kitega uchumi kuacha mara moja na kujituma katika miradi mbalimbali ili waweze kutengeneza pesa yao wenyewe, lakini pia hii itasaidia katika kutunza afya zao na kujithamini na kujiheshimu na kuufanya mwili kuwa mali yako na si mali ya kila mtu mwenye pesa.
Tabia ya wadada warembo kutembea na waume za watu kutembea na wapenzi wa watu imekithiri hivyo wafike mahala wajitambue na watumie uzuri wao kwa utashi ili wasiharibu maisha ya watu wengine kama kuvunja ndoa za watu na n.k.