Afara Suleiman – Hanang’, Manyara.

Mlima Hanang ni mlima mkubwa uliopo katika Mkoa wa Manyara nchini Tanzania. Hanang ni mlima wa volkeno ikiwa volkeno ya kusini zaidi kati ya zile zilizopo nchini Tanzania na wenye kipenyo cha kilomita 10-12 na urefu wa mita 3,417 juu ya usawa wa bahari.

Mkoa huu wa Manyara, una milima mingi ambayo ni pamoja na Milima ya Bokwa, Kidero, Lelatema, Meri, Ndaleta, Sangaiwe, Soui, Dara, Gidahaida, Giyeda Mara, Hanang, Hassama, Kwaraha, Leya, na Ol Doinyo Lolbene, na kwa kanda ya kati Mlima Hanang’ ndiyo mlima mrefu zaidi.

Mwezi Novemba 2022 Wakala wa Misitu Tanzania – TFS, Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara ulisheherekea miaka sita tangu Hifadhi ya Mlima Hanang ipandishwe hadhi, huku kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 11, 2022 watalii zaidi ya 1,500 wakitembelea hifadhi hiyo iliyoko kaskazini mwa Taifa la Tanzania.

Kupitia sherehe hizo, tukafahamu pia idadi hiyo ya watu wanaoupanda Mlima Hanang imekuwa ikiongezeka kila siku kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ile ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha ambazo zimeboresha miundombinu katika hifadhi ya mlima huo kunzia geti la kuingilia, vyoo vya kisasa na njia za kuelekea juu ya mlima.

Watanzania, ndani na nje ya nchi hatuna budi kutenga muda na kupanda mlima huo wenye sifa nyingi za kuvutia ikiwemo mandhari nzuri kiasi ambacho kilipelekea Mlima huo kupandishwa hadhi ya kuwa hifadhi ya Taifa Novemba 11, 2016 na pia ifahamike kuwa Mlima huu nne kwa urefu nchini Tanzania.

Katika hifadhi hiyo, pia kuna maporomoko ya maji na shughuli za kijamii za kabila la warbabaig (Tara), wanaotoka maeneo mbalimbali yakiwamo Balangdalalu, Gehandu na Dirma na wao hufika eneo hilo la mlima kuabudu yaani ‘Qadwe’, wakitumia mapango na miti mikubwa kufanya ibada za kijadi na matambiko.

Dkt Mollel: Madaktari Wazalendo 2,469 wamesajiliwa
Makatibu SADC wakutana kwa dharula hali ya Ulinzi, Usalama