Heldina Mwingira.

Kiziwi ni mtu yeyote ambaye uwezo wake wa kusikia Sauti aidha umepungua au umeisha kabisa na neno hili Kiziwi pia hutafsirika kwa maana isiyopishana na ya awali kwamba Kiziwi ni mtu ambaye hawezi kusikia kabisa au hawezi kusikia vizuri, ikijulikana kama kupoteza usikivu.

AINA YA VIZIWI

Kuna aina tofauti za Viziwi, ikiwemo (1) Kiziwi kwa kuzaliwa, huyu ni mtu yeyote ambaye amezaliwa akiwa kiziwi na hajawahi kusikia sauti yoyote au lugha yoyote ya kusikia (2), kiziwi kabla ya kupata lugha, ambaye ni mtu yeyote aliyezaliwa anasikia lakini amepoteza uwezo wake wa kusikia.

Hii ni kabla hajapata lugha ya kusikia, hivyo alipata kidogo lugha mama na alijifunza kidogo lugha hiyo mama na ndugu wa familia na (3), kiziwi baada ya kupata lugha ambaye ni mtu yeyote aliyezaliwa na uwezo wa kusikia lakini alipoteza uwezo wake wa kusikia baada ya kuwa ameshajifunza na kujua lugha ya kusikia na kuongea vizuri.

Lugha ya alama ni lugha ya kuona inayotumia ishara na hisia za uso katika kuwasiliana.

Aidha, ni vizuri kufahamu na kutofautisha makundi hayo tajwa ya viziwi hapo juu, ili uelewe vizuri kwanini wapo viziwi ambao wana uwezo mzuri wa kuongea na wapo wengine ambao uwezo wao wa kuongea ni mgumu, hawaongei maneno yanayoeleweka au sentensi zao wakati mwingine hazipo sahihi.

LUGHA YA ALAMA

Lugha ya alama ni lugha ya kuona inayotumia ishara na hisia za uso katika kuwasiliana na zipo namna za kufanya ishara tofauti kwa kutumia Mishale inayoonesha namna ambavyo unapaswa kuelekeza mikono yako wakati wa kufanya kila ishara ili kuelewana na Kiziwi.

Muhtasari huu wa somo la Lugha ya Alama ya Tanzania – LAT, umeandaliwa kutokana na Mtaala wa Mafunzo ya Ualimu Elimu Maalumu wa mwaka 2019, ukilenga kumjengea Mwalimu tarajali maarifa, stadi na mwelekeo utakaomwezesha kukabiliana na mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji wa mwanafunzi kiziwi aliyedahiliwa katika elimu ya msingi.

Love

Tukumbuke kwamba Kiziwi hutumia lugha ya alama kama njia yao kubwa ya mawasiliano na wapo viziwi wenye uwezo mkubwa wa kusoma mdomo lakini matatizo yao ya kusikia husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kuzeeka, kelele, ugonjwa au kemikali na maumivu ya kimwili nk.

Kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya Mwaka 2012, zinaonesha kuwa ya Nchini Tanzania kuna viziwi zaidi 425,000 ambao ni sawa asilimia 0.97 ambapo pia zipo changamoto kubwa inayowakuta viziwi ni changamoto ya mawasiliano kuanzia ngazi ya familia mpaka kwenye jamii inayowazunguka.

CHANGAMOTO

Katika kuangazia changamoto hiyo, Dar24 Media imeangazia changamoto wanayoipata jamii ya Viziwi hasa zile ambazo wanakutana nazo mara kwa mara, ambapo kwa upande wao Wafanyabishara wanasema ipo changamoto katika mawasiliano wakati wa utoaji wa huduma mbalimbali.

Kutakuwa na ulazima wa Walimu wote tarajali kusoma somo la Lugha ya alama katika huu mtaala mpya.

Mfanyabiashara wa eneo la Mwananyamala jijini Dar es Salaam, Joseph Mushi yeye anasema, “tunapata changamoto kubwa katika kuwasiliana nao kwa kutumia lugha ya alama kwani binafsi kama mimi siijui ila ili niweze kuelewana naye inanilazimu kumuangalia usoni.”

MTAALA

Serikali Nchini imepanga kuijumuisha lugha ya alama kwenye mitaala ya elimu ikilenga kutatua changamoto za mawasiliano zinazowakabili Wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, ambapo mchakato wa mapitio ya sera na mitaala unaendelea na somo hilo limependekezwa kuwa la lazima.

Kutokana na changamoto hiyo Mkalimani wa Lugha ya alama, Heldina Mwingira alimtafuta Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Nchini – TET, Dkt. Aneth Komba ambaye alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya lugha kwa watu hao wenye tatizo la kusikia akisema, ” tumeandaa kamusi Lugha ya Alama ambayo itasaidia, ni ya bure na hata mtandaoni inapatikana.”

Amesema, “kutakuwa na ulazima wa Walimu wote tarajali kusoma somo la Lugha ya alama katika huu mtaala mpya na tumehakikisha kwamba somo la Lugha ya Alama limependekezwa kuwa somo la lazima kwa walimu wote tarajali, ili tuweze kuhakikisha lengo linafikiwa.”

Kiziwi ni mtu yeyote ambaye uwezo wake wa kusikia Sauti aidha umepungua au umeisha kabisa.

Dkt. Komba anaongeza kuwa, Dira ya elimu na mafunzo inasisitiza kuwapo kwa mwalimu aliye bora kitaaluma na kitaalamu na mwenye mbinu mbalimbali za kujifunzia na kufundishia somo la Lugha ya Alama ya Tanzania ili kukabiliana na changamoto za mahitaji na matarajio ya kielimu kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

“Mwelekeo wa dira na mpango wa elimu kwa ujumla ni kumwandaa mwalimu mwenye ujuzi na stadi za Lugha ya Alama katika shule za msingi kwa kuzingatia misingi, kanuni na mielekeo inayopasa. Mwalimu tarajali wa somo la Lugha ya Alama kwa ajili ya Mwanafunzi kiziwi anayehitaji kupata ujuzi wa kuyatumia vyema mazingira yake katika kuwezesha mawasiliano,” anasisitiza Dkt. Komba.

Kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya Mwaka 2012, zinaonesha kuwa ya Nchini Tanzania kuna viziwi zaidi 425,000 ambao ni sawa asilimia 0.97. Picha ya Reuters.

MAONI

Ili kumsaidia mkufunzi, yametolewa mapendekezo ya mbinu za kufundishia na kujifunzia, zana/vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na upimaji. Mkufunzi anahimizwa kutumia mbinu mbalimbali na zana zinazopatikana kwenye mazingira yanayohusika na upimaji ulioshauriwa.

Pamoja na mbinu mbalimbali za kufanikisha somo hili kwa kutumia mbinu zilizoainishwa kwenye kitaalamu, pia mkufunzi anaweza kutumia mbinu nyingine tofauti kulingana na mazingira na mahitaji ya mwalimu tarajali na umahiri unaojengwa ili kuelewana na Kiziwi.

Hivyo, Dar24 Media pia ilipata maoni kutoka kwa Mwanafunzi wa Shule Jumuishi, Editha Krisensi ambaye anasoma na Wanafunzi ambao ni Viziwi, yeye anasema uwepo wa Mtaala uliopendekezwa utasaidia kuwezesha mawasiliano mazuri kati yao na wepesi wa kuelewana tofauti na ilivyo sasa.

Alama hii huamanisha neno amen / amua.

“Hii itasaidia na itatufanya sisi ambao hatujui Lugha ya Alama, tutafundishwa na itakuwa rahisi kuwasiliana na marafiki zangu wawili ambao ni viziwi lakini si mimi tu hata watu wengine sasa wataweza kuelewana nao na kubadilishana kimawazo ya mambo mbalimbali yanayotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku hasa masomo,” alisema Editha.

MUAFAKA

Ni wazi kuwa, Taasisi ya Elimu Tanzania – TET, kuweka somo la Lugha ya Alama kuwa la lazima vyuoni kwa walimu tarajali itasaidia baada ya Walimu kuajiriwa kuwafundisha Wanafunzi ambao sio viziwi hivyo itasaidia kutatua changamoto ya mawasiliano kati ya wasio viziwi na Viziwi katika shughuli mbalimbali za jamii.

Dira ya elimu na mafunzo inasisitiza kuwapo kwa mwalimu aliye bora kitaaluma na kitaalamu na mwenye mbinu mbalimbali za kujifunzia.

Hii inatokana na ukweli kuwa, Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa walimu wa Elimu maalum na wasio wa elimu maalum 3,650 wa shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna bora ya kuwafundisha na kuwahudumia wanafunzi viziwi, ili kujenga jamii jumuishi ya viziwi shuleni.

Elimu inayotolewa ni ya kurithisha maarifa, stadi na mielekeo bora kutoka kwa vizazi vilivyopita hadi vizazi vya wakati huu na vijavyo, hivyo, malengo makuu ya elimu nchini ni kuendeleza na kukuza maendeleo, kuboresha haiba ya wananchi wa Tanzania, rasilimali zao na matumizi bora ya rasilimali hizo katika kuleta maendeleo ya mtu binafsi na ya kitaifa.

Msitumie nguvu fuatilieni maendeleo ya Watoto - ACP Abwao
Simamieni urithishwaji wa ujuzi kwa Wazawa - Rais Samia