Kutokana na hali ya uchumi kubadilika kuna baadhi ya biashara zinadorora, kwa mujibu wa wafanya biashara mbalimbali wamelalamikia sekta zao kushuka kibiashara kwa asilimia kubwa kulingana na miaka ya nyuma ambapo biashara hizo zilikua zikifanya vizuri.

Ambapo wamiliki wamesema kuna baadhi ya huduma ambazo walikuwa wakizitegemea kutengeneza pesa hazifanyiki, mfano biashara ya hoteli imedorora kutokana na baadhi ya huduma kukosa wateja ikiwemo kukodisha kumbi kwa ajili ya mikutano, miaka ya nyuma kumbi zilikuwa zinafanya vizuri mikutano mingi ilikua inafanyika katika mahoteli makubwa tofauti na sasa.

Mfano Hoteli nyingi maeneo mengi zimefungwa na nyingine kugeuzwa kuwa mambweni.

Hata shughuli za ujenzi katika maeneo mengi zimeshuka kwa kasi sana kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu, wafanya biashara ya matofali, vigae,  mbao, rangi, bidhaa za ndani wanalalamika kuwa biashara imekuwa mbaya hela hakuna ujenzi katika viwanja vingi mjini umesimama.

Kwa upande wa biashara ya nguo, miaka ya nyuma  ilikua ikifanya vizuri sana hasa katika msimu wa sikukuu hali imekua tofauti miaka ya hivi karibuni kwani sikukuu sio tena siku ya kuvaa nguo mpya hali ya maisha imepanda kiasi cha kubadilisha mwenendo wa maisha ya watu.

Biashara ya chakula kwa mbali inafanya vizuri nahii ni kutokana na hitaji hilo kuwa ni hitaji muhimu katika maisha ya kila mwanadamu, japo wamo ambao kwa siku wananshindia mlo mmoja au kukosa kabisa mlo hii ni kutokana na hali ya maisha kuwa juu kiasi cha kuwashinda wahusika.

Wafanyabiashara wanatakiwa kuenda na upepo wa soko lilivyo ili kukidhi matakwa ya wateja wa bidhaa zao.

Serikali itazame swala hili kwa jicho la tatu na kupambanua na kuchanganua mapungufu yaliyopo katika kukidhi mahitaji ya maisha ya kibinadamu.

 

Kiungo wa Chelsea apata ajali
Trump aongeza vikwazo Korea Kaskazini, Kim Jong-un ajibu