Kama ulikuwa unaamini kuwa beki wa pembeni wa klabu ya Liverpool, Trent Alexander-Arnold ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuliko wachezaji wote watakaoshiriki fainali za kombe la dunia mwaka huu 2018, ulikosea.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye alionesha umahiri mkubwa wakati wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kuwa sehemu ya kuifikisha Liverpool fainali ya msimu wa 2018, ameteuliwa kuwa miongoni mwa wachezaji 23 watakaoitumikia England wakati wa fainali za kombe la dunia zitakazoanza Juni 14 nchini Urusi.
Baada ya kutangazwa kwa ikosi vya mataifa mengine yatakayoshiriki fainali za mwaka huu, imebainika Trent Alexander-Arnold ni mchezaji anaeshika nafasi ya tano kwenye orodha ya wachezaji 10 wenye umri mdogo waliotajwa kwenye timu zao za taifa, tayari kwa fainali za kombe la dunia.
Wanaomtangulia Trent Alexander-Arnold wana umri sawa wa miaka 19, lakini wmaepishana miezi, jambo ambalo linaendelea kudhihiridha kuwa beki huyo kinda wa Liverpool ni mkubwa kuliko waliomfuatia kuzaliwa kwenye orodha hiyo. Kweli kila ‘mdogo ana mdogo wake!’.
Mchezaji Daniel Arzani wa timu ya taifa ya Australia, ambaye ni shabiki mkubwa wa Alexander-Arnold, atakuwa mchezaji mdogo zaidi kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu.
Arzani mwenye umri wa miaka 19 tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Australia, na mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya Jamuhuri ya Czech uliochezwa juma lililopita.
Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kwenye klabu ya Melbourne City FC inayoshiriki ligi ya nyumbani kwao Australia (A-League), anatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha Socceroos.
Anayemfuatilia ni mshambuliaji machachari wa klabu bingwa nchini Ufaransa PSG, Kylain Mbappe, ambaye atakuwa mchezaji anayeshika nafasi ya pili kwenye orodha ya wenye umri mdogo zaidi kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu.
Mbappe alizaliwa siku 15 baada ya uzawa wa Arzani.
Mshambuliaji huyo aliyeitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya UFaransa, tayari ameshajijengea umaarufu mkubwa katika soka duniani, kufuatia uwezo na umahiri wake uwanjani, lakini kilichombeba hadi kufahamika zaidi ni uhamisho wake wa mkopo kutoka AS Monaco kwenda PSG mwanzoni mwa msimu wa 2017/18 uliogharimu kiasi cha Pauni milioni 168.
Kwa msimu wa 2017/18 Mbappe aliifungia PSG mabao 21.
Makinda hawa watano watawasha moto kwenye viwanja mbalimbali vya soka nchii Urusi kuanzia kesho kutwa. Wakiwa na nafsi ya kushiriki mitanange mingi zaidi kutokana na umri wao, historia watakayoiandika kwenye fainali za mwaka huu zitakuwa na maana kubwa kwenye safari yao.
Endelea kuifuatilia Dar24, tutakujuza mengi kuhusu Kombe la Dunia, usiache kuendelea kuifuatilia Channel yetu ya YouTube ya ‘Dar24 Media’ tukusogeze Urusi.
ORODHA YA WACHEZAJI WENYE UMRI MDOGO KWENYE FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2018. | |||
MCHEZAJI | UMRI | TEREHE YA KUZALIWA | NCHI |
Daniel Arzani |
19 | 04.01.1999 | Australia |
Kylian Mbappe |
19 | 20.12.1998 | Ufaransa |
Achraf Hakimi |
19 | 04.11.1998 | Morocco |
Francis Uzoho |
19 | 28.10.1998 | Nigeria |
Trent Alexander-Arnold |
19 | 07.10.1998 | England |
Moussa Wague |
19 | 04.10.1998 | Senegal |
Jose Luis Rodriguez |
19 | 19.06.1998 | Panama |
Ian Smith |
20 | 06.03.1998 | Costa Rica |
Ismaila Sarr |
20 | 25.02.1998 | Senegal |
Lee Seung-woo |
20 | 06.01.1998 | Korea Kusini |