Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameelekeza ulipaji wa fidia ya wananchi Mto Ng’ombe ufanyike Jumatatu ya wiki ijayo baada ya taratibu zote kukamilika.

RC Makalla ameyasema hayo alopokutana na watendaji wa taasisi mbalimbali zikizopo ktk mkoa wake kwa lengo la kufahamiana, kupokea taarifa na changamoto.

Utekelezaji wa ulipaji wa fidia wananchi mto Ng’ombe ni kufuatia agizo la katibu mkuu wa CCM, Daniel chongolo alilolitoa tarehe 22 mwezi huu kwa Mkuu wa Mkoa kulifuatilia suala hilo na kulipatia ufumbuzi ndani ya wiki moja.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 27, 2021
Simba SC yaendelea kutetea ASFC