Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kingo za fukwe za bahari zilizopo jijini Dar es salaam ili kuweza kujionea hatua iliyofikiwa.

Amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa fukwe hizo kutasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, pia kuweza kuondokana na madhara ambayo yanweza kutokea wakati wa mvua ambapo kumekuwa kukitokea mafuriko ya mara kwa mara.

Aidha, amesema kuwa Serikali ina mpango wa kuweka mradi mkubwa katika mto msimbazi ili uweze kuwa kivutio kikubwa jijini Dar es salaam tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo mto huo umekuwa kama dampo la kutupia takataka.

“Majiji mengi duniani yana mito mikubwa inayokatiza na ni vivutio vikubwa sana kwa sababu watu husafiri kwenda kutalii kwenye majiji hayo, sasa na sisi tunampango wa kuubadili mto msimbazi ili uwe kivutio kikubwa duniani, watu wawe wanakuja kwaajili ya kutalii katika mto huu,”amesema Makamba

Hata hivyo, Makamba ameongeza kuwa mto huo ni rasilimali kubwa ambayo kama ikitumiwa vizuri na kutunzwa, basi taifa litafaidika na mapato ambayo yatatokana na shughuli ambazo zitakuwa zikifanyika.

 

Video: Makonda agawa Computer katika manispaa za jiji la Dar
Video: Prof. Lipumba amnanga Maalim, ataka Bashange ashughulikiwe