Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, January Makamba amemwomba Spika Job Ndugai kusimamia Bunge liwe lenye tija kwa taifa na kutokuwa na Bunge linalojadili watu na maisha yao binafsi.
Amezungumza hayo akijibu hoja za wabunge walizotoa katika bajeti ya Serikali leo bungeni Juni 26, 2018 Makamba ameanza kwa kusema wabunge wamemshabulia Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango na si Wizara.
”Wakati mwingine mezani kuna hoja lakini tunajadili mambo binafsi na mimi nimemfahamu Dk Mpango miaka kumi nyuma, hii habari ya kiburi mimi binafsi na wengine tunaokutana hii haipo na ndani ya Bunge tupingane kwa hoja lakini tunapomwendea binafsi tunakuwa tunakosea,” amesema Makamba.
Mimi namtetea Mpango namfahamu na ukiondoa taratibu zake za kusikia ila ni msomi na amefanya kazi ndani na nje ya nchi”. ameongezea Makmba.
Makmba amesema hata Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji anafahamika na katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk James Dotto anafahamika lakini ni vyema kuwatia moyo kwa weledi wao.