Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba amesema kuwa sifa pekee ziwaendee waasisi wa Taifa, Julius Nyerere na Abeid Amani Karume kwa kulitetea taifa hadi kufika hapa lilipo.

Ameyasema hayo kwenye mkutano mkuu wa tisa wa Chama cha Mapinduzi mara baada ya Mwenyekiti wa muda Benjamin William Mkapa kumpa nafasi ya kuwasalimia wajumbe na wageni waliohudhuria mkutano huo.

”Tunajipongeza sisi tunasahau waliotengeneza nchi, waasisi Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume, lakini vile vile nampongeza Rais Magufuli kwa kufanya kazi bila woga, anafanya kazi kwa weledi mkubwa sana,”amesema Makamba.

Aidha, amesema kuwa alishawahi kutabiri kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alikuwa akibatiza kwa kwa maji lakini Rais Dkt. Magufuli anabatiza kwa moto kitu ambacho kwa sasa kinatokea.

Hata hivyo, Makamba amewatahadharisha wapinzani kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hautokuwa rahisi kwao kwani Chama Cha Mapinduzi kimejipanga vizuri kuweza kushinda tena.

 

Video: Ni Magufuli, Vigogo watano watumbuliwa NHC
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 19, 2017