Wakati timu yake ya zamani ya Yanga ikipangwa na waarabu kutoka Misri timu ya Pyramids FC, Heriter Makambo na timu yake ya Horoya AC wamepangiwa kucheza dhidi ya timu ya Bandari kutoka Kenya.

Makambo anayeitumikia Horoya AC ya Guinea, walitolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kutupwa katika mechi za mtoano za Kombe la Shirikisho Afrika sawa na Yanga.

Wakati Makambo akielekea Kenya, timu yake ya zamani Yanga itaanza kibarua cha raundi ya kwanza dhidi ya Pyramids FC kutoka Misri jijini Mwanza.

Horoya AC waliondolewa na JS Kabylie ya Algeria huku Yanga ikitolewa na Zesco United kutoka Zambia.

Video: Rugemalira awasha moto mpya sakata la Escrow, Makombora ya Kikwete yatikisa
Waziri Hasunga akerwa kasi ya ujenzi wa Vihenge