Taaasisi ya kupambana na Rushwa, imemfungulia mashitaka ya ufisadi Makamu wa rais nchini Malawi, Saulos Chilima, kufuatia kashfa ya kumpa rushwa mfanyabiashara mwenye asili ya Uingereza na Malawi.
Taasisi hiyo, imesema Chilima ambaye tayari amevuliwa mamlaka yake amekuwa akihusishwa na madai kadhaa ya ufisadi katika kushawishi zabuni za serikali.
Kiongozi huyo, alifikishwa mahakamani jana mchana (Novemba 25, 2022) na wafuasi wake kutoka chama cha United Front Movement walikusanyika nje ya jengo la Mahakama kuonyesha kumuunga mkono kiongozi wao.
Hata hivyo, Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera alimvua mamlaka Chilima mapema mwezi Juni, 2022 baada ya madai hayo kufichuliwa kwa mara ya kwanza.