Makamu wa rais nchini Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amezindua kondomu isiyo na kelele na yenye ladha ya machungwa kwa wabunge  wa nchi hiyo.uzinduzi huo umefanyika bungeni nchini Afrika kusini.

Cyril Ramaphosa alielezea kwamba mipira hiyo ya kondomu ilitengenezwa kufuatia malalamiko kwamba kondomu za serikali zilikuwa zina harufu mbaya na kelele.

Tangazo hilo la Ramaphosa lilizua hasira na tabasamu kutoka wanachama wa ANC na kelele kutoka kwa upinzani wa chama cha EFF huku baadhi ya wanachama wake wakisema ”mpatie Zuma hizo”.

Matamshi hayo ya wanachama wa EFF yanatoka miaka 10 iliyopita wakati bwana Zuma alipokiri kwamba katika kesi yake ya ubakaji ,alifanya mapenzi bila kutumia mipira ya kondomu na mwanamke aliyekuwa na virusi vya HIV.

Aliondolewa mashtaka hayo lakini kukiri kwake kulizua mshangao mkubwa nchini humo ambapo takribani watu milioni saba wana virusi

Wizara ya Elimu yatakiwa kuandaa wataalamu wakutosha
Picha: Majaliwa katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Answar, Msasani