Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman ameitaka jamii kuendelea na malezi mema ili kupata vijana wenye maadili wanaoweza kuitumikia jamii na kuwa na kasi ya wanaoweza kuisaidia kasi ya upatikanaji wa maendeleo ya nchi.
Othman ameyasema hayo katika kijiji cha Masipa Pamndani wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akitoa salamu zake kwa wakazi wa Kijiji hicho, baada ya kushiriki futari ya pamoja aliyoandalia.
Amesema, “jami imekumbwa na janga kubwa la ukosefu wa uadilifu katika vyombo mbali mbali ikiwemo mahakama na mamlaka nyenginezo na hivyo kuchangia watu kukosa haki zao kutokana na watendaji waliowengi kukosa maadili kunakochangiwa na kutoshikamana na maadili mema.”
Othman yupo Pemba kwa ziara ya siku nne ambapo pamoja na kutembelea wagonjwa katika wilaya zote pia alishiriki futari ya pamoja iliyowashirikisha wananchi, Viongozi wa siasa na serikali wa mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba.