Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Urithi Festival akimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika tamasha hilo ambalo litazinduliwa Septemba 15 uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Satano Mahenge wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini Kwake, amesema tamasha hilo halitakuwa na kiingilio chochote.
”Tamasha hilo litakuwa na maonyesho mbalimbali ya ngoma za Asili za Mkoa wa Dodoma na jirani na pia kutakuwa na burudani za aina yake kutoka kwa wasanii wa ndani na nje hivyo wananchi nawaomba wajitokeze kwa wingi kushuhudia utamaduni wao kutoka sehemu mbalimbali” amesema Dkt. Mahenge.
Aidha, amesema kuwa tamasha hilo linafanyika Dodoma kutokana na Serikali kuamua kuhamishia Ofisi zote za watumishi hivyo ni mwendelezo wa kujenga Dodoma mpya na kutakuwa na fursa mbalimbali kwa watu wa Jiji hilo.
Vilevile Dkt. Mahenge amewapongeza waandaaji wa tamasha hilo ambao ni Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mkoa wa Dodoma ambapo watu wataona watu wakicheza ngoma za makabila yao jinsi yanavyotunza Urithi toka kwa jamii zao.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Prof. Audax Mabulla amesema kuwa tamasha hilo litafanyika kila mwaka, na kutakuwa na maadhimisho ya kilele cha Urithi Festival kwa Watanzania wote.
Dkt. Mabulla amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vitu mbalimbali kutoka kwenye Makumbusho na pia kutakuwa na uchomaji wa nyamapori na watu wataweza kununua na kula kwa bei ya kawaida.
Pia ameitaja Mikoa itakayofuatia kuonesha tamasha la Urithi Festival baada ya Dodoma kuwa ni Zanzibar, Mwanza, Dar es salaam na Mwisho itakuwa mkoa wa Arusha hivyo kwa upande wao kila kitu kimekamilika kinachosubiriwa na siku ya tamasha