Makamu wa kwanza wa Rais nchini Sudan Kusini, Rieck Machar na mkewe ambaye pia ni waziri wa ulinzi, Angelina Teny wameambukizwa virusi vya Corona ambavyo vinasababisha ugonjwa wa covid -19.

Taarifa kutoka ofisi ya Machar iliyothibitishwa na msemaji wake James Gatdek Dak, imeeleza kuwa Machar, mkewe pamoja na watumishi kadhaa wa ofisi yake na walinzi pia wamekutwa na maambukizi.

Machar mwenyewe ametoa taarifa kwa umma kwamba ameambukizwa virusi vya corona na kuanzia leo atajiweka karantini kwenye makazi yake kwa siku 14 zijazo. 

Kulingana na takwimu za wizara ya afya ya Sudan Kusini zilizotolewa hapo jana, hadi sasa kumerekodiwa visa 339 vya COVID-19 na vifo sita.

 Mashirika ya misaada yamekuwa yakielezea wasiwasi kuhusiana na kuongezeka kwa haraka kwa visa hivyo katika siku za karibuni nchini humo.

Miaka sitini jela kwa kubaka mwanafunzi
Said Ndemla akubali kubaki Simba SC