Makamu wa raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania ameahidi kuwa serikali itanunua mashine mbili za kisasa za mionzi kwa ajili ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zita saidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa matibabu kwa wagonjwa katika Taasisi hiyo.
Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi hiyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea Taasisi  hiyo pamoja na Kumtembelea na kumpa pole Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhani Feruzi ambaye anapatiwa matibabu kwenye Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.                                                                                                                                                                          
Aidha Mh.Suluhu amesisitiza kuwa mkakati uliopo wa serikali unalenga kuhakikisha kuwa hali ya utoaji wa huduma za afya na dawa kote nchini unaimarika maradufu ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwenye maeneo yao kwa ubora unatakiwa.

Kuhusu uhaba wa wahudumu wa afya katika Taasisi hiyo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi uongozi wa Taasisi hiyo kuwa serikali itahakikisha wahudumu hao wanapatikana katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

  Katika hatua nyingine baadhi ya wagonjwa na wananchi wamepongeza utoaji wa tiba katika Taasisi hiyo na wameomba serikali iendelee kuipatia vifaa vya kisasa vya kutolea huduma kama hatua ya kuboresha utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wa saratani.

Makonda, Malinzi Kupamba Uzinduzi Airtel Rising Stars Kesho
Azam FC Wamalizana Na Winga Wa Medeama SC