Aliyekua kiungo wa klabu ya Chelsea na Real Madrid Claude Makelele amekua sehemu ya benchi la ufundi la klabu ya Swansea City, ambalo linaongozwa na meneja Paul Clement.
Makelele ana ukaribu na Clement na inaaminiwa wataweza kufanya kazi nzuri na kufikia lengo linalokusudiwa huko kusini mwa nchini Wales yalipo makao ya klabu ya Sanswea City (Liberty Stadium).
Makelele mwenye umri wa miaka 43, alikua msaada mkubwa katika kikosi cha Chelsea wakati akicheza soka, jambo ambalo liliisaidia klabu hiyo ya Stamford Bridge kutwaa ubingwa wa kwanza msimu wa 2004/05, baada ya miaka khamsini.
Makelele alifanya kazi na Chelsea, akisajiliwa kutoka kwa magwiji wa soka wa mjini Madrid, Real Madrid.
Baada ya kuondoka magharibi mwa mwa jijini London, Makelele alirudi nchini kwao Ufaransa na kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain, na alipotangaza kustaafu, akawa sehemu ya benchi la ufundi chini ya utawala wa Carlo Ancelotti.
Kwa mara ya kwanza Makelele ataonekana katika benchi la ufundi la Swansea City akisaidiana na Clement, mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Arsenal.