Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anna Makinda amewashauri madiwani wanawake kuhakikisha wanajenga hoja zitakazozifanya halmashauri zao kuwatambua wanawake walio nje ya mifumo ya kifedha ili kuwasaidia kupata mikopo inayotolewa kupitia fungu la uwezeshaji.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa asilimia kumi ya fedha zinazotengwa na kila halmashauri nchini zimelenga kuwainua kiuchumi wanawake hao ambapo hawapo kwenye vikundi kama VICOBA, SACCOS na aina nyingine za makundi ya kijasiriamali.
Amesema kuwa njia nyingine ambayo madiwani wanawake wanaweza kuitumia ni kupitia mabaraza ya madiwani ambako wanatakiwa kutoa ushauri wa kuongeza vyanzo vya mapato.
Hata hivyo, ameongeza kuwa asilimia kumi inayotengwa kuinua wananchi kiuchumi iwe ya kutosha na kuwafikia wahitaji wengi zaidi wanahitajika kupaza sauti zao.