Uongozi wa Simba SC umethibitisha kukamilisha mchakato wa kuwanasa makocha watatu wapya kwa ajili ya kuboresha Benchi la Ufundi la timu hiyo kwa ajili ya kusaka mafanikio ya msimu ujao 2023/24.

Majuma mawili yaliyopita Simba SC ilitangaza kuachana na Kocha wa makipa Zakaria Chlouha, Kocha wa viungo, Kelvin Mandla na mtaalamu wa viungo, Fareed Cassim, hivyo ilianza mchakato wa kuziba nafasi za watu hao kwa mujibu wa matakwa yaliyoelekezwa na Mkuu wa Benchi la Ufundi Robertinho.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa makocha waliowapata wako vizuri na wamjiridhishwa kuwa wana uwezo mkubwa wa kusaidiana na Kocha Mkuu, ambaye ana jukumu la kuipa Ubingwa timu yao msimu ujao 2023/24.

Ingawa Ahmed Ally hakuwa tayari kubainisha maelezo mengine juu ya kupatikana kwa makocha hao, amesema mashabiki wa timu hiyo wasiwe na wasiwasi kwani ni makocha wazuri na wenye weledi mkubwa wa utendaji wa kazi zao.

“Kwa sasa tumeshapata wataalamu wote hao watatu kwa maana pia kocha wa viungo ambaye yuko vizuri sana, na ubingwa unaanzia kwenye utimamu wa wachezaji, kama una wachezaji legelege maana yake hawatakuwa na uwezo wa kumudu dakika 90 au watakuwa na majeraha kila wakati,” amesema Ahmed

Amesema wana Imani na makocha hao, wanafahamu kiu ya mashabiki na wapenzi wa Simba SC ya kuhitaji mafanikio kuanzia msimu ujao hivyo nao wamefanya jambo stahiki katika hilo.

Aidha, Ahmed amesema kuwa bado wanaendelea na mazungumzo na wachezaji wengine ambao wataachana nao na kwamba hawajamaliza zoezi hilo licha ya kwamba wameshawatema wachezaji saba mpaka sasa.

Klopp apewa mchongo wa usajili Liverpool
AC Milan yajitosa tena kwa Loftus-Cheek