Makomando watatu wa vikosi maalum vya Jeshi la Marekani wameuawa katika oparesheni dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Niger.

Taarifa iliyotolewa na komandi ya Marekani iliyoko barani Afrika, imeeleza kuwa makomando wengine wawili walijeruhiwa vibaya katika shambulizi la kushtukiza linaloaminika kufanywa na wapiganaji wa Al-Qaeda karibu na mpaka wa Mali, Jumatano iliyopita.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Makomando hao walikuwa miongoni mwa wakufunzi waliokuwa wakitoa mafunzo kwa vikosi vya Niger kuhusu mapambano dhidi ya wapiganaji wa makundi ya kigaidi katika eneo hilo.

Maafisa wa Jeshi la Marekani wameeleza kuwa majeruhi walikimbizwa katika jiji la Niamey ambalo ni Makao Makuu ya nchi hiyo na kwamba hali yao kiafya inaimarika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Trump alipewa taarifa kuhusu tukio hilo alipokuwa anajiandaa kuelekea Las Vegas kwenye eneo ambalo watu 59 waliuwa na mtu mwenye silaha kwenye tamasha la muziki.

Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou amelaani shambulio hilo akieleza kuwa wanajeshi kadhaa wa Niger ni miongoni mwa waliouawa na kujeruhiwa.

Rais Issoufou hakutaja idadi ya wanajeshi wa Niger walioua au kujeruhiwa kwenye tukio hilo.

Ndugai awanong'oneza mawaziri wateule
Peter Crouch aingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia