Vyombo vya dola nchini Somalia vimeeleza kuwa makomando wa Marekani pamoja na Makomando wa nchi hiyo wamefanikiwa kuwakamata watu watatu wanaoaminika kuwa ni makamanda wa kundi la kigaidi la Al-Shaabaab baada ya kufanya oparesheni kali katika kijiji kimoja.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa watu watano ambao ni wakulima wa ndizi walipoteza maisha katika oparesheni hiyo.
Afisa wa kitengo cha Intelijensia ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kuwa makomando hao walilenga kituo maalum cha Al-Shabaab ambacho kinatumika kama kiungo cha mawasiliano.
Kiongozi wa kimila wa kijiji hicho, Moalim Ahmed amesema kuwa makombando hao pia waliwakamata baadhi ya wanakijiji.
Kamandi ya Marekani barani Afrika haijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.
Kundi la Alshabaab ambalo ni mshirika wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda linaendesha oparesheni dhidi ya Serikali ya Somalia, likitaka kusimika utawala sheria kali za kidini.
Marekani ni moja kati ya nchi zilizotoa msaada wa kijeshi nchini humo kupambana na wanamgambo wa Al-Shabaa.