Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameendelea kumshukuru Diamond Platnumz ambaye amabye ni bosi wa WCB kwa kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wikii hii na kutoa msaada kwaajili ya watoto wenye matatizo ya moyo.
Mwanamuziki huyo alifanikisha kukusanywa Sh 84 milioni kwa ajili ya matibabu ya watoto 500 ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo. Matibabu ya mtoto mmoja ni shilingi milioni 2..
Makonda kupitia Instagram amesema atumuunga mkono muimbaji huyo kwa kwenda kwenye tamasha la Wasafi festival, ambalo linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam.
“Diamond Platinumz umeweka alama kubwa sana moyoni mwangu , hata kama Mvua itanyesha nakuhakikishia nitakuja na kuushuhudia upendo wako kwa watoto wa kitanzania abao umeokoa maisha yako,” ameandika Makonda kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo, Makonda amekuwa akiendesha kampeni ya kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kitengo hicho cha moyo, kuwa kuna watoto zaidi ya 500 wameshindwa kutibiwa kutokana na gharama za matibabu.