Kutokana na kusuasua kwa kukamilisha miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na hospitali kwa wakati, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Mkonda, amemwagiza katibu tawala wa mkoa Abubakar kunenge pamoja na wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafuta likizo zote za mwisho wa mwaka kwa watendaji wakuu wa idara za Afya.
Makonda ametoa uamuzi huo baada ya kubaini utendajikazi mbovu katika miradi ya Afya kwenye wilaya za Kigamboni na Temeke huku wakuu wa idara hizo wakionekana kutoendana na kasi ya utendaji kazi ya Rais Dk. John Magufuli.
“Rais aliingiza katika akaunti shilingi milioni 500 lakini hazikufanyakazi yeyote na wiki mbili zilizopita aliingiza shilingi bilioni moja katika akaunti, bado hakuna kilichofanyika” makonda alisema alipokuwa wilayani kigamboni.
Nakuongeza kuwa nijambo la kusikitisha kuona halmashauri imeingiziwa fedha zote za kujenga hospitali kubwa, lakini watendaji wa idara hiyo hawajihangaishi kuanza ujenzi, “wananionyesha kiwanja watakapojenga hospitali, mimi nilidhani mmeanza hatakung’oa nyasi, tangu julai mwaka huu fedha zipo katika akaunti lakini mganga mkuu anazungukatu”
Aidha Makonda amemtaka Kunenge kufuatilia utendaji kazi wa watendaji hao na ikiwezekana kumwandikia ripoti, atakayowasilisha katika mamlaka za juu ili kuangalia uwezekano wa kuwatimua au kuwapangia majukumu mengine.