Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amehaidi Kuijengea nyumba ya vyumba vinne familia ya mwandishi (mpiga picha) wa magazeti ya Serikali TSN wanaochapisha Magazeti ya Habari Leo na Daily News Marehemu Athumani Hamis aliyefariki dunia na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Dkt. Yonaz kwa niaba ya Makonda ambae aliombwa kuisadia familia ya marehemu ambayo ina watoto Wanne wanaosoma huku wakiwa wanaishi kwenye nyumba ya kupanga kutokana na Baba yao kuugua kwa zaidi ya miaka 10.

Aidha, Dkt. Yonaz amesema kuwa kwa kutambua mchango wa tasnia ya habari hususani waandishi wa habari amekubali kujenga Nyumba hiyo kama kielelezo cha Kumuenzi Marehemu Athumani ambae katika uhai wake alikuwa Mpiga Picha Mahiri wa Magazeti ya Serikali nchini.

Hata hivyo, hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na baadhi ya waandishi wa habari ambao wamesema Kitendo cha Makonda kukubali Kuijengea nyumba familia hiyo ni kitendo cha kijasiri na kinapaswa kuigwa na viongozi wengine.

JPM amjulia hali Mzee Kingung'e Hospitali ya Muhimbili
Majaliwa aagiza maafisa kilimo kuingia shambani