Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, leo Agosti 03 amekabidhi Ofisi rasmi kwa Mkuu mpya wa Mkoa huo Abubakar Kunenge aliyeteuliwa July 15 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na kushuhudiwa na waandishiwa, watumishi wengine wa ofisi hiyo pamoja na Kamanda wa polisi kandaa maalum Lazaro Mambosasa.

Kabla ya kukabidhi nyaraka mbalimbali za ofisi huyo, Makonda alimshukuru Rais Magufuli kwa kipindi chote alichomuamini na kumkabidhi Mkoa wa Dar es Salaam kama Mkuu wa Mkoa na mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama.

“Nitaendelea kumuenzi Rais John Pombe Magufuli kama jemedali wangu” Alisema.

mbali na pongezi na shukurani kwa Rais Magufuli, Makonda akamshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Kunenge, kuendelea kuwaacha wafanyabiashara wa vyombo vya usafiri (Boda Boda na Bajaji) kuendelea kuingia mjini, ili kujipatia kipato cha kila siku, huku akimtaka kutosahau watoto Yatima, wanawake Wajane na Wasiojiweza.

Uteuzi wa Makonda ulitenguliwa na Rais Magufuli baada ya kiongozi huyo mstaafu kuingia kwenye mchakato wa kuomba ridhaa ya kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Kigamboni.

Mikael Arteta amnyatia Rakitic
Maximo aomba kurudi Young Africans