Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda ametembelea na kukagua wa Ujenzi wa Daraja la JPM (Kigogo – Busisi), lenye urefu wa Kilomita 3 na Barabara unganishi yenye urefu wa Kilomita 1.66 linalojengwa Wilayani Misungwi.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemueleza Mwenezi Makonda kuwa Ujenzi wa Daraja hilo umefikia asilimia 80.

Aidha, amesema mpango wa Serikali ni kuhakikisha hadi kufikia mwezi Agosti 2024 ujenzi huo utakuwa umekamilika kwa asilimia.
Mwenezi Makonda pia ameitaka Serikali kuhakikisha inaongeza kasi katika utekelezaji wa Mradi huo.