Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda katika harakati za kusuluhisha matatizo mbalimbali yanayowakumba wakazi wa Dar ameeleza kuwa amekutana na changamoto kubwa ya wakazi wa hao kudhrumiwa mali na wajanja wachache wanaotumia utalaamu wa sheria au fedha walizonazo kuwakandamiza wanyonge na kuwanyima haki zao.
Amesema katika Serikali ya Magufuli Kwa kudra za mwenyezi Mungu atalisimamia swala hilo na kupigania haki za wananchi wanyonge waliokwisha kudhurumiwa mali zao walizopata kihalali.
Hivyo amewatangazia wakazi wa Dar kuanzia januari 29, 2018 mpaka febuari 2, 2018 wafike katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa , wote waliodhurumiwa na kunyanyasika kwa kunyimwa haki zao huku wakiwa na nyaraka halali za umiliki wa mali walizodhurumiwa.
Ambapo amesema ataandaa jopo la wanasheria ambao atakaa nao na kupitia kesi ya mmoja baada ya mwingine ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mwananchi aliyedhurumiwa.
‘’Watakaobainika kweli ni wamiliki halali na nyaraka zao ni halali serikali yenu chini ya magufuli itasimama upande wenu kuhakikisha mnarudishiwa mali zenu’’ amesema Makonda.
Hivyo amewaomba wakazi wote wa Dar kuhakikisha wanafika katika ofisi ya mkuu wa mkoa na nyaraka zao kumaliza utata uliojitokeza.
Aidha ameomba taarifa hii kuisambaza kwa watu wote jijini Dar es salaam ambao tayari wamekwisha teseka kwa muda mrefu bila kupata suluhisho ya mali zao na ameahidi kuwa Serikali ya magufuli nisuluhisho tosha.