Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametimiza ahadi yake aliyoahidi siku ya hafla ya kuichangia klabu ya Yanga maarufu kama ‘KUBWA KULIKO’ ambapo aliahidi kuipatia uwanja klabu hiyo.

Makonda amekabidhi nyaraka za uwanja huo uliopo Kigamboni jijini Dar es salaam kwa mwenyekiti wa klabu hiyo. Mshindo Msola na kuwahakikishia umiliki halali wa uwanja huo.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Makonda amesema kuwa makabidhiano hayo yanatoa ishara nzuri kwamba serikali ina nia ya dhati ya kukuza michezo.

”Jumamosi iliyopita niliahidi kuwa nitaipa klabu ya Yanga uwanja eneo la Kigamboni na leo tumeanza mchakato wa kuwamilikisha rasmi ili waanze ujenzi wa uwanja wao,”amesema Makonda

Kwa upande wake kaimu katibu mkuu wa Yanga, Omary Kaaya amemshukuru mkuu wa mkoa na serikali kwa ujumla kwa kuwapatia uwanja huo.

 

Mwanamazingaombwe apotelea mtoni akifanya onyesho
Video: Jeshi lenye Nguvu na Tishio zaidi Duniani

Comments

comments