Shirika la uzalishaji mali la Jeshi la kujenga Taifa (suma JKT), limepewa kazi ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ubungo.

Kazi hiyo wamepewa na leo Oktoba 29, 2019 na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye amesema kuwa ujenzi huo unatakiwa kamilika kwa miezi mitatu.

Amebainisha hayo leo alipotembelea eneo itakapojengwa hospitali hiyo Kimara Baruti, ambapo aliambatana na viongozi wengine na kuangalia jinsi maandalizi mbalimbali yalivyoanza kufanyika.

Makonda ametoa shukurani zake kwa mara nyingine tena kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kukubali ombi lake la sh 1.5 bilioni za ujenzi wa hospitali hiyo.

” Wilaya hii ni mpya inahitaji viongozi shupavu wa kuwaletea maendeleo, ni kazi ya viongozi wanaochaguliwa na wananchi”. amesema Makonda

“kwa bahati mbaya Ubungo ilipata viongozi wanaojali matumbo yao tu. Hata leo hapa hawapo ila kesho watakuja na maneno matamu ili muwape kura” Ameongeza Mkuu huyo wa mkoa.

Mkurugenzi mtendaji wa Suma JKT, Kanali Rajabu Mabele amesema kuwa watahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.

 

Makonda: Ubungo hatujapata viongozi wa maendeleo, bali wa matumbo yao
Ujio wa Mapadri waliooa utafanikiwa?