Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demnokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu amesema aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hapaswi kuwa uraiani kwani kuna makosa ya jinai ambayo aliyafanya wazi, ikiwemo kuwanyamg’anya watu magari na nyumba.

Lissu ameyabainisha hayo wakati akifanya Mahojiano maalum na Dar24 Media nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kusema hayo yote yana ushahidi na umeonekana akitolea mfano uvamizi wa kituo cha Redio na Luninga vinavyomilikiwa na Clouds Media.

“Makonda amefanya uhalifu mwingi sana, amevamia kituo cha clouds, kunyang’anya watu majumba, kunyang’anya watu magari na makosa mengine chungu mzima na ushahidi upo, hana tofauti na Sabaya, akina Sabaya wapo wengi mtaani na hawafai kuwepo huko wanatakiwa wawe Gerezani,” amesema Lissu.

Aidha, Lissu amesema, suala la kumshughulikia Sabaya peke yake linaleta taswira kuwa huenda zipo sababu zingine kwani waliofanya makosa mfanano naye wapo wengi na hajui kwanini imekuwa katika hali hiyo kitendo kinachozalisha maswali mengi.

Atta Agyei achimba mkwara Ligi Kuu 2023/24
Kilipuzi chaokotwa, chauwa tisa