Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na mkewe Marry Massange wamezuiliwa na serikali ya Marekani kuingia nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Januari 31, 2020 na wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeeleza kuwa mkuu huyo wa mkoa pamoja na mkewe wamezuiwa kutokana na tuhuma za kushiriki kukandamiza haki za binadamu nchini Tanzania.
Taarifa hiyo inafafanua kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu Makonda alioufanya jijini Dar es salaam ni pamoja na kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na usalama wao.
” Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki za binadamu kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es salaam” inasema taarifa hiyo.
Mbali na taarifa hiyo iliyotolewa kwa urefu, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Michael Pompeo ametumia akaunti yake ya Twitter kutangaza zuio hilo.