Leo Septemba 15, 2018 katika bandari ya jijini Dar es salaam kumefanyika mnada wa makontena 20 yaliyoingizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kwa mara ya nne mfululizo yamekosa tena wanunuzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scolastica Kevela, akizungumza katika mnada huo amesema mnada umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana.

Aliongeza kwamba hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazikidhi malengo yaliyowekwa na kwamba wao kama  madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.

”Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo wametaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa” amesema Scolastica.

Makontena hayo 20 ambayo ndani yake kuna vifaa vya shule ikiwa ni pamoja na vifaa vya ofisi za walimu.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewahi kuonya mtu yeyote atakayejitokeza kununua makontena hayo na kudai kuwa atalaaniwa yeye na uzazi wake.

Makontena hayo 20 yalikuwa miongoni mwa makontena 80 yaliyokuwa yamenasa bandarini kwa kutolipiwa kodi.

Barabara za juu Tazara zaanza kutumika rasmi leo
Mama Muna afunguka mazito ya Muna, ''Muna ameniua''