Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanya mnada tena kwa mara ya tatu mfululizo wa makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lakini yameshindwa kuuzika kutokana na wateja kushindwa kufika bei.

Mnada huo umefanyika bandari kavu ya Dar es salaam (DICB), ikiwa ni mwendelezo wa minada miwili iliyofanyika huko nyuma lakini hakuna hata kontena moja ambalo limefanikiwa kununuliwa.

Aidha, TRA imepanga bei ya shilingi milioni 60 kwa kila kontena lakini wateja wameshindwa kufikia bei hiyo, wengi wakifika shilingi milioni 20 hadi 30.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kivela amesema kuwa wao kama madalali wanafanya jukumu lao kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa na TRA, hivyo hawawezi kupunguza bei bila maelekezo ya mamlaka ya mapato.

“Kila mnada wateja wanajitokeza lakini wanaishia bei zilezile za milioni 20 mpaka 30 kwahiyo mzigo huu wa samani haununuliki labda mpaka tupate maelekezo mapya kutoka TRA,” amesema Kevela

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 9, 2018
Huyu ndiye mkuu wa mkoa bora kwangu- JPM