Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Hamad Masauni ameweka hadharani makosa yanayoweza kumsababishia mtu kukaa mahabusu kwa muda wa masaa 24 ametaja makosa hayo kuwa ni;
- Uhaini
Hili ni kosa la jinai, Katika kifungu cha 39 (1) a,b,c,d,e, na F kimetaja kuwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mtu yeyote atakayejaribu kumuua rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kujenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, au kufungwa kwa rais, kumwondoa rais madarakani visivyo halali, kumwondolea rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali atakuwa ametenda kosa la uhaini na ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kupindua serikili iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama atakuwa ametenda kosa la uhaini na adhabu yake huwa ni kifo ikiwa itathibitika mahakamani
2 Ujambazi wa kutumia silaha
3 Mauaji
4 Kujihusisha na biashara za dawa za kulevya
5 Ugaidi
6. Usafirishaji wa fedha haramu
7. Mtuhumiwa aliyehukumiwa kifungo kinachozidi miaka mitatu
8. Aliyewahi kuruka dhamana
Aidha, Kisheria ukubwa wa kosa hupimwa kwa adhabu yake, kosa likiwa kubwa mtuhumiwa hutumikia adhabu kubwa vivyo hivyo kosa likiwa dogo mtuhumiwa huadhibiwa kiasi.
Hivyo endapo utakutwa na hatia ya makosa yaliyoorodheshwa hapo juu sheria itachukua mkondo wake na mtuhumiwa ataadhibiwa mkabala na kosa lake.