Serikali Nchini Rwanda, imesaini makubaliano na shirika la Canada na Ujerumani, ili kuanzisha ujenzi wa kinu cha nyuklia kitakachoanza majaribio mwaka 2026.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Dual Fluid Energy, Goetz Ruprecht amewaambia Waandishi wa Habari jijini Kigali kuwa aina mpya ya vinu hivyo, vinaweza kutumiwa kuzalisha umeme, haidrojeni na mafuta yaliyosindikwa kwa gharama ndogo kuzidi mafuta ya visukuku.

Kituo cha Nishati cha Nyuklia cha Callaway. Picha ya AMEREN Missouri.

Aidha, Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Ernest Nsabimana amesema matumizi ya Nishati ya Nyuklia yatakua ni chanzo cha kuaminika cha umeme, kupunguza utegemezi wa mafuta na kusaidia kukidhi mahitaji ya Nishati.

Amesema, “Nyuklia katika jumla ya vyanzo vya nishati kutapelekea kuwa na aina mbalimbali za vyanzo vya nishati, kuimarisha usalama wa nishati na kupunguza hatari ya uhaba wa usambazaji.

La Saba kujipima ya miaka saba kielimu
Spika kuanzisha uchunguzi kutokuwa na imani na Rais