Mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia chama cha ACT Wazalendo, Saed Kubene, anatarajia kufungua kampeni zake za kuwania nafasi hiyo kesho jumapili Septemba 27, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mratibu wa uchaguzi wa ACT Wazalendo jimbo la Kinondoni Leila Madibi, mkutano wa kumnadi Kubenea, utafanyika kwenye viwanja vya Buibui, vilivyopo Mwananyamala.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mgombea huyo amechelewa kufungua kampeni zake kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo kufunguliwa kesi ya jinai mkoani Arusha.

“Kesho ndio tunaanza mchakamchaka wa siku takriban 35 za kutafuta uungwaji mkono wa wananchi wa Kinondoni,” amesema Leila ambaye amewahi kuwa diwani katika manispaa za Kinondoni, Ubungo na jiji la Dar es Salaam kati ya mwaka 2015 na Juni 2020.

Leila ameeleza kuwa mbali na uzinduzi huo wa kampeni hizo za kuwania ubunge, mkutano huo utahudhuriwa na kiongozi mkuu wa chama hicho Zitto Zuberi Kabwe ambaye anatarajiwa kueleza kile kinachoitwa ” Makubaliano ya ushirikiano wa kimyakimya, kati ya ACT – Wazalendo na CHADEMA.Katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 Kubenea anakabiliana na mgombea wa Chama cha mapinduzi (CCM), Abbas Tarimba.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 27, 2020
Lukuvi akanusha viongozi kupora ardhi