Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Profesa Abel Makubi ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa imetakiwa kukamilisha ujenzi wa Jengo la huduma za wagonjwa mahututi na dharura ifilapo mwezi November Mwaka huu.
Ameyasema hayo leo Septemba 21, 2021 wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Iringa, huku akisisitiza kukamilika kwa mradi huo ili uanze kutoa huduma ifikapo mwezi Novemba 2021.
“Hongereni kwa kukaribia kumaliza hili jengo na sasa mkamilishe hatua za mwisho ili huduma zianze kutolewa Novemba 2021,” Amesema Prof Abel Makubi,
Aidha Profesa Makubi amesema kuwa Kumalizika kwa Jengo hilo la Wagonjwa mahututi na dharua , ni matokeo ya juhudi za Serikali ya awamu ya chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, na limegharimu shillingi milioni 600.
Prof. Abel Makubi pia ametembelea Maabara, wodi za wagonjwa na huduma za nje (OPD) ,na kuongea na Wananchi kuhusu Kampeni za kutekeleza mpango wa Jamii Shirikishi na harakishi wa kuhamasisha Wananchi kuchanja katika halmashauri mbalimbali nchini.