Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limepanga Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani humo msimu huu 2023/24, huku mchaka mchaka kwa timu shiriki katika hatua hiyo ukitarajiwa kuanza Novemba 26.
CAF imepanga makundi hayo mjini Johannesburg-Afrika Kusini leo Ijumaa (Oktoba 06), chini na Mkuu wa Idara ya Mashindano ya Shirikisho hilo, Khalid Nassar.
Bingwa wa michauno hiyo msimu wa 2022/23 USMA Algers kutoka Algeria amepangwa Kundi A sambamba na Future (Misri), Super Sports United (Afrika Kusini) na Al Hilal (Libya).
Kundi B: Zamalek SC (Misri), Sagrada Esperança (Angola), Académie SOAR (Guinea) na Abu Salim (Libya).
Kundi C: Rivers United (Nigeria), Club Africain (Tunisia), Dreams FC (Ghana) na Académica do Lobito (Angola).
Kundi D: RS Berkane (Morocco), Diables Noirs (Congo Brazzaville), Stade Malien (Mali) na Sekhukhune United (Afrika Kusini).