Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo litapanga makundi na ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani humo, kwa msimu wa 2020/21.

Hafla ya upangaji wa makundi na ratiba ya michuano hiyo, itafanyika mjini Nyon nchini Uswiz yalipo makao makuu ya UEFA, na kuhudhuriwa na maafisa wa UEFA pamoja na viongozi wa klabu shiriki.

Msimu wa michuano ya Ligi ya mabingwa Barani Ulaya hatua ya mtoano ulianza rasmi Agosti 08 hadi Septemba 30, huku hatua ya makundi ya michuano hiyo ikitarajiwa rasmi Oktoba 20 na mchezo wa fainali utachezwa 29 Mei 2021 kwenye Uwanja wa AtatĂĽrk Olympic, mjini Istanbul nchini Uturuki.

Timu 32 zilizofuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo zimepangwa kwenye vyungu vinne tofauti, na kisha zitaenguliwa moja moja ili kuunda makundi manane ya michuano hiyo.

CHUNGU CHA KWANZA: Bayern Munich, Sevilla, Real Madrid, Juventus, Paris Saint-Germain, Liverpool, Zenit na FC Porto.

CHUNGU CHA PILI: FC Barcelona, Atletico Madrid, Manchester United, Manchester City, Chelsea, Borussia Dortmund, Ajax na Shakhtar Donetsk.

CHUNGU CHA TATU: Inter Milan , SSC Lazio, Atalanta, RB Leipzig, Olympiacos, Dynamo Kiev, Red Bull Salzburg na Krasnodar.

CHUNGU CHA NNE: Lokomotiv Moscow, Marseille, Club Brugge, Borussia Monchengladbach, Rennes, Istanbul Basaksehir, Ferencvaros na Midtjylland.

Tetesi: Guendouzi kurudi Ufaransa, Houssem Aouar kusajiliwa Arsenal
Azam FC waiandalia dozi Kagera Sugar