Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ametoa siku 45 kwa wawekezaji wa mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kudhibiti vumbi linalosambaa na kusababisha kero kwa wananchi.

Dkt. Jafo ametoa maagizo hayo Aprili 04, 2023 wakati wa ziara ya kikazi kwa lengo kukagua na kujioenea hali halisi, kujadili hatua stahiki zinazofaa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi huo na toa muda huo kwa wawekezaji hao kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia ili waweze kuondoka na kupisha mradi huo vinginevyo utasitishwa kuendelea na shughuli zake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Bahi Godwin Gondwe.

Amesema, “nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakililamika kupata vumbi kutokana na shughuli inayofanyika hapa na tume iliundwa hapa na watu wa madini na kutoa maelekezo lakini hawakufuata sasa hatuwezi kuvumilia watu hawa hawafuati sharia za nchi, maelezo yangu ni hayo mawili vingine mradi huu utafungwa,” alisisitiza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe alisema alimshukuru Waziri Jafo kwa kufika katika eneo hilo na kusikiliza na kushughulikia changamoto hizo na kuahidi kuyasimamia maelekezo aliyotoa ili na kuhakikisha wawekezaji hao wanatekeleza maelekezo hayo ndani ya siku 45 ambazo Waziri Jafo ametoa ili kuhakikisha madhara ya vumbi hayawafikii wananchi.

Eneo la mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma unafanyika na kulalamikiwa na wananchi kuleta changamoto ya kusambaa kwa vumbi.

Awali, baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakiwemo Diwani wa Kata ya Mundemu Stanley Mtati, Bw. Richard Nyagani walisema wamekuwa wakipata kero ya milipuko inayotumika kulipua mawe ambayo inaletea madhara yakiwemo kuharibika kwa nyumba.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)- Kanda ya Kati kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Dodoma na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi, hivi karibuni ilifanya Ukaguzi katika eneo la mradi huo.

Amir Khan astaafu masumbwi kwa aibu
Arsenal, Man City kazi bado mbichi England