Mahakama kuu nchini Malawi imetoa amri ya kupinga agizo la serikali la wananchi wote kukaa ndani kwa muda wa siku 21 kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Jaji wa Mahakama kuu, Kenyatta Nyirienda amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya shirika la kupigania haki za binadamu nchini humo kupeleka pingamizi kwa madai kuwa serikali inatakiwa kupanga mikakati kwaajili ya masikini kwanza kabla ya kuwakataza kutoka nje.
Kabla Mahakama haijatoa amri hiyo, wafanyabiashara wadogo (machinga), pamoja na vijana wadogo walikuwa wameandamana katika miji mikubwa kupinga amri ya kukaa ndani iliyotolewa na Rais, wakidai kuwa wapotayari kupata corona kuliko kufa kwa njaa.
Mtanzania akutwa na corona Uganda
Jumanne wiki hii Rias wa nchi hiyo, Peter Mutharika alitangaza amri ya kukaa ndani kwa wiki tatu ambayo ilitarajiwa kuisha Mei 9, akitaadharisha kuwa kama hawatakuwa makini watu elfu 50 wanaweza kupoteza maisha.
Nchi ya Malawi hadi sasa imethibitisha visa vya wagonjwa wa corona 17 huku wamwisho akiwa na miaka 70 , mfanyabiashara mwenye asili ya bara la Asia.