Baada ya saa 24 za kuapishwa Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, amemuondolea kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Peter Mutharika.

Amewataka Mawaziri kurudisha mali za Serikali na amemfuta kazi Mkuu wa Polisi, Duncan Mwapasa na kumteua Inspekta Jenerali Dkt. George Kainja kuchukua nafasi hiyo.

Ikumbukwe kuwa, akiwa Rais, Peter Mutharika hakufuta baraza lake la Mawaziri ingawa alitakiwa kufanya hivyo siku chache kabla ya uchaguzi kama ambavyo Katiba ya Malawi inamtaka kufanya.

Mawaziri waliokuwa katika Baraza lake wametakiwa kurudisha mali zote za Serikali wanazozishikilia yakiwemo magari waliyopewa na Serikali hadi kufikia siku ya kesho kabla ya saa tano asubuhi.

Wachambuzi wa siasa wanaamini kuwa katika kipindi hiki kigumu haswa, maamuzi magumu yatahitajika kuhakikisha mambo yanaenda, ukiachia uhusiano wa changamoto ya virusi vya corona, lakini pia kuna suala la kukabiliana na rushwa na kukuza kwa uchumi.

CORONA: CAF yafanya maamuzi michuano ya Afrika
Magufuli adhaminiwa na wanaCCM milioni 1.02