Mahakama ya juu nchini Malawi imeiamuru serikali kuruhusu wanafunzi wanaosuka mtindo wa marasta (dreadlocks) kwenda shule.

Uamuzi huo wa muda ulitolewa wakati mahakama inaendelea kusikiliza kesi iliyofunguliwa na mwanafunzi mmoja ambaye alikataliwa kuanza shule ya msingi kwa sababu ya nywele zake.

Kulingana na tovuti ya shirika la habari la Nyasa, mamlaka ya shule ilimtaka mwanafunzi huyo kukata nywele zake kwanza ndipo aanze masomo.

Lakini hakimu wa mahakama kuu nchini Malawi aliagiza shule hiyo impokee mwanafunzi huyo na kumpa usaidizi wa ziada katika masomo yake kwa siku zote ambazo hakuruhusiwa kuingia darasani.

Gazeti la The Nation , la nchini humo limeripoti kuwa Jamii ya marasta nchini humo imekuwa ikiituhumu serikali kwa ubaguzi dhidi yao.

Mambo 6 yaliyomuumiza Mabeste baada ya ndoa yake Kuvunjika ''Nilitamani kufa"
TBS yakanusha taarifa zinazosambaa kuhusu kinywaji cha ukwaju