Chama cha soka nchini Malawi (FAM) kimetangaza kuziondoa timu za taifa kwenye mchakato wa kufuzu fainali za Afrika za 2019, pamoja na zile za mataifa bingwa barani humo (CHAN) za mwaka 2018.

FAM wametangaza maamuzi hayo, kufuatia sakata la ukosefu wa fedha za maandalizi kwa timu zao za taifa, ambazo kwa kiasi kikubwa bajeti yake hutolewa na serikali ya nchi hiyo.

Katibu mkuu wa FM,  Alfred Gunda amesema viongozi wa chama hicho wamejadili kwa kina ili kusaka ufumbuzi wa kuzinusuru timu zao za taifa zishiriki fainali za Afrika, lakini imeshindikana.

Amesema lengo lao lilikuwa ni kutaka kuiona Malawi inakua sehemu ya timu zitakazosaka nafasi ya kushiriki fainali za CHAN na zile za AFCON, lakini kila walipojaribu kusaka mbinu mbadala kwa kuishirikisha serikali ya nchi hiyo mambo yalikwama.

Hata hivyo, kiongozi huyo amewataka wadau wa soka nchini Malawi kuelewa suala hilo kama lilivyowasilishwa katika vyombo vya habari, na halitokua jambo la busara kuanza kulaumu na kuwaona viongoziwa FAM kama wamefanya kusudi.

Katika hatua nyingine, Gunda amesema Malawi ipo tayari kulipa faini ambayo itatangazwa na CAF kwa maamuzi waliyoyachukua,  kuliko wakiingia kwenye michuano na wakalazimika kujiondoa kati kati.

Thesis Statement Illustrations for Research Papers
Rais Dkt. Magufuli: CCM haitambembeleza mtu