Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock atatumia ziara yake barani Afrika wiki kesho kurudisha sehemu ya kazi za sanaa zilizoibwa enzi ya utawala wa kikoloni nchini Nigeria.
Msemaji wa Mwanadiplomasia huyo, amesema Baerbock anayesafiri kwenda Nigeria hapo kesho Jumapili Desemba 18, 2022 atabeba kazi 20 za sanaa zinazofahamika kama “Vinyago vya shaba vya Benin” na kuzikabidhi kwa serikali jijini Abuja.
Aidha, kurejeshwa kwa vinyago hivyo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa mapema mwaka huu baina ya nchi hizo mbili, kwa Taifa hilo la Ujerumani kukabidhi nchini Nigeria kazi za kale za sanaa zipatazo 514.
Hata hivyo, vinyago hivyo ni miongoni mwa turathi zilizoibwa mwaka 1897 na kundi la wapelelezi wa ukoloni wa Uingereza, kutoka kwenye kasri la ufalme wa Benin, eneo ambalo sasa ni kusini magharibi mwa Nigeria.