Nchini Mali viongozi wa mapinduzi ya kijeshi wamefanya mazungumzo na viongozi wa upinzani ambao wamepongeza kung’olewa madarakani kwa Ibrahim Boubacar Keïta pamoja na Waziri mkuu huku viongozi wa nchi za afrika magharibu wametangaza kufunga mipaka yao na nchi hiyo

Muungano wa upinzani umesema unatambua utashi wa jeshi na kuundwa kwa serikali ya mpito ya kiraia ambapo wamemlaumu kwa kushindwa kukomesha mashambulio ya jihad na kuporomoka kwa uchumi wa nchi.

Kanali wa jeshi Assimi Goita, amejitokeza kama kiongozi mpya wa jeshi la nchi hiyo na kuwataka wafanyakazi wa umma kurejea kazini.

Viongozi wa Afrika Magharibi wwanatarajia kufanya mkutano kwa njia ya video na kujadili hatua zaidi dhidi ya Mali.

Orodha ya waliopitishwa kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM, Gwajima, FA wapeta
Bwalya afurahia anachokiona Simba SC