Mwenyekitu wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatius Balile amesema miongoni mwa changamito ambayo vyombo vya habari nchini inapitia, licha ya sheria ambayo ipo katika mchakato wa maboresho ni pamoja na malimbikizi makubwa ya madeni ya vyombo vya habari.

Ameyasema hayo wakati wa Kongamano la Kwanza la Maendeleo ya Sekta ya Habari lilofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa JNICC.

Kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo ya Rais Samia la kuwataka wadau wa vyombo vya habari kukutana ili kujadili kuhusu maendeleo ya sekta hiyo.

Hivi karibuni Rais Samia alisema Serikali itavilipa vyombo vya habari deni la zaidi ya shilingi bil. 6 baada ya kufanya uhakiki wa deni hilo ambalo ni moja ya mambo aliyosababisha kufa kwa baadhi ya vyombo vya habari.

Rais Samia alitoa ahadi hiyo Juni 28, 2021 wakati akijibu swali la Mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile aliyeomba Rais kutimiza ahadi yake iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ya kulipa deni hilo kabla ya June 30, 2021.

Balile amesema licha ya juhudu kufanywa bado yasisi za serikali zikiwemo halmashauri havijalipa madeni yao kwa vyombo vya habari.

“Mpaka mwishoni mwa mwaka jana madeni amabyovyombo vya habari vinadai kwa serikali na taasisi zake bil.7 ukijumuisha na denila gazeti la Daily News la serikali bil. 11 jumla ya deni ni bil.18 na zaidi”

Marekebisho ya Sheria ya Habari kufanyika Januari 2023
Balile: Sheria ikirekebishwa Uhuru wa habari utapatikana