Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), kutokana na kifo cha Rais wa zamani wa FIFA, Joao Havelange aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.

Katika salamu hizo, Rais Malinzi amesema amepokea taarifa za kifo cha Joao Havelange kwa masikitiko makubwa akimkumbuka zaidi pale aliongeza washiriki wa kombe la dunia kutoka timu 16 hadi 32, ambapo mashindano 6 yalifanyika chini ya utawala wake.

Joao Havelange, raia wa Brazil alikuwa mtangulizi wa Sepp Blatter katika shirikisho la mpira wa miguu duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998. Blatter alijiuzulu nafasi ya Urais wa FIFA Aprili, 2013 kutokana na ripoti ya uchunguzi wa madai ya kupokea rushwa.

Joao Havelange aligua kwa muda mrefu na kulazwa hospitali tangu mwaka 1999 alipokumbwa na ugonjwa wa mapafu.

Alikuwa mmoja wa wanakamati wa Olimpiki (IOC), kuanzia mwaka 1963 hadi 2011 alipojiuzulu kwa sababu ya kudhoofu kwa afya yake. Havelange aliiwakilisha Brazil katika mashindano ya Olympic ya Kuogelea mwaka 1936, mwaka ambao aliidhinishwa kuwa mwanasheria kabla ya kuchaguliwa na IOC.

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Joao  Havelange mahala pema peponi. Bwana alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.

TFF Yatibua Uchaguzi Wa Chama Cha Soka Dar es salaam (DRFA)
Video: Waziri Mkuu awaweka sawa watumishi wa Ofisi yake